Nafasi Ya Matangazo

July 15, 2014

a.KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda wa pili kulia akiwa anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya ziara yake katika mkoa wa Arusha
b.
Waandishi wa habari wakiwa kazini
KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda amewataka wazee wa kimila (malwaigwanan), viongozi wa dini pamoja na wazazi kutumia muda wa ziada  kukaa na vijana wao na kukemea kuacha mara moja kutumiwa katika vitendo viovu vinavyoendelea mkoani hapa.

Alisema kuwa , vijana wengi  wamekuwa wakituhumiwa kufanya  uhalifu  wa  ulipuaji wa mabomu jijini hapa ambapo wengi wao ni vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 25.

Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi pamoja na vijana katika wilaya ya Arusha na Meru wakati alipotembelea  maeneo hayo kwa lengo la kujionea hali halisi ya vijana na kuzungumza nao.

Alisema kuwa, mkoa  wa Arusha hivi sasa unakabiliwa na wakati mgumu sana kutokana na uvunjifu wa amani unaofanywa na vijana kwa kutumiwa na baadhi ya watu kwa lengo ya kuvuruga amani ya mkoa wa Arusha na kwa nchi kwa ujumla.

Mapunda alisema kuwa, wazee wa kimila pamoja na viongozi wa dini wana mchango mkubwa sana katika jamii inayowazunguka hivyo wakiweza kuwakutanisha vijana na kuzungumza nao kuhusiana na kutokukubali kutumiwa katika uvunjifu wa amani badala yake wawe walinzi wa nchi yao na kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu.

‘jamani mkoa wa Arusha una vivutio vingi sana vya watalii ambavyo kwa ujumla vimekuwa vikiingizia mkoa wa Arusha fedha nyingi pamoja na taifa kwa ujumla , na pia kupitia vivutio hivyo vijana wengi wameweza kupata ajira na hata wengine kujiajiri sasa tunapofikia hatua ya kujiingiza kwenye uvunjifu wa amani ,hata uchumi unayumba kwani hakuna atakayependa kutembelea Arusha tena’.alisema Mapunda.

Alifafanua zaidi kuwa,ni vizuri vijana wakawa mstari wa mbele kuwafichua wale wahalifu wanaovunja amani badala ya kuwakumbatia na kuwapa ushirikiano  hali ambayo inachangia uchumi wa nchi kuyumba kwa ujumla.

Mapunda  aliwataka wadau mbalimbali nchini kushirikiana na  kuwa walinzi  katika maeneo yao ikiwemo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maeneo husika pale watakapowabaini wahalifu mahali popote ili tuweze kuinusuru nchi yetu badala ya kuachia swala la ulinzi kwa jeshi la polisi peke yake.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,Robinson Meitinyiku alisema kuwa,kutokana na matukio ya uhalifu wa mabomu yanayoendelea jijini hapa seriakli itaendelea kuchukua wajibu wake na kuhakikisha kuwa amani inadumushwa.

Alisema kuwa, wao kama uvccm mkoa wa Arusha wamekuwa wakiwaomba wazee wa kimila pamoja na viongozi mbalimbali kukaa na vijana na kuweza kuwasihi kutokubali kutumiwa katika uhalifu huo.(Pamela Mollel wa jamiiblog)
Posted by MROKI On Tuesday, July 15, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo