Nafasi Ya Matangazo

April 29, 2014

Baloziwa Tanzania chini Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano la Biashara na uwekezaji katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja Nigeria ikiwa nisehemu yasherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Teddy Mapunda akizungumza wakati Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu  vivutio  vya utalii vya Tanzania katika kongamano la biashara na uwekezaji jijini Abija Nigeria juzi.(Na Mpigapicha wetu


Mh. Daniel Ole Njoolay, Baloziwa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku akishuhudiwa na mwakilishi wa  rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wapilikulia) na baadhi mabalozi wanao wakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa na ubalozi wa Tanzania kusherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika hotel ya Sheraton jijini Abuja Nigeria.
*********
Na Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria
Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza kwa ujumla na kutembelea vivutio vya utalii mbalima livinavyopatikana nchini Tanzania.

Hayo ya mesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria nakufanyika katika Hoteliya Sheraton jijini Abuja.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la Biashara naUwekezaji, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay amesema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa la Tanzania Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimia miaka 50.

“Watanzania tuna jivunia sana muungano wetu kwani niwakipekee sana hapa barani Afrika, nani muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano wowote ule Barani Afrika” alisema Balozi Njoolay.

Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka amesema kwamba mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizimbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara katiyake na Nigeria. 

Naye Mkurugenzi wamipango na maendeleo wa mamlakaya EPZ Bwana Lamau Mpolo ameelezea uwepowa fursanyingi za uwekezaji katika sektambalimbali ikiwemo ya gesi na madini.  Ameelezea pia namna serikaliya Tanzania ilivyoweka mazingira mazuri kwaajili ya kuvutia  wawekezaji kutoka duniani kote katika sekta mbalimbali za uchumi nchini Tanzania.

Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu ya 7 yaasili barani Africa, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Bibi Teddy Mapunda amesema pamoja na vivutio vitatu (3) vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya asili barani Afrika, vivutio vingine nihifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi ya Taifa ya Kituro, hifadhi ya Taifa ya Gombena Pori la akiba la Selous.

Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wavivutio vya Tanzania sambamba na kuwekeza katikasekta ya utalii.

Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Nigeria mia moja lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli hiyo n akuhudhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa mataifambalimbali nchi Nigeria, wagenikadhaa mashuhuri na baadhi ya watanzania waishio nchini Nigeria.
Posted by MROKI On Tuesday, April 29, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo