Nafasi Ya Matangazo

April 19, 2014

Washiriki wa Miss Tabata 2014 wakiwa mazoezini Da’ West Tabata.
 *********
Na Mwandishi Wetu
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano la kusaka mrembo wa Tabata 2014, watatambulishwa leo katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
 
Utambulisho huo utaenda sambamba na uzinduzi wa Redds Miss Tanzania Tabata. 
 
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga alisema jana utambulisho huo utaenda sambamba na kusherekea sikukuu ya Pasaka.
 
Kapinga alisema bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi huo utakaojumuisha pia washiriki wa Miss Ukonga na Miss Mzizima wa mwaka huu.
 
Pia Kapinga alisema kuwa Twanga Pepeta pia itatumia utambulisho huo kutambulisha nyimbo zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
Alisema bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.
 
Mratibu huyo alisema wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao leo kabla hawajashiriki kwenye shindano la kumsaka Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao. 
 
Pia watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa pamoja na Miss Tabata Dorice Mollel. 
 
Washiriki wa Miss Tabata ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18),  Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
 
Wenine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20)
 
Warembo hao wanafundishwa na Neema Chaki na Pasilida Bandari. Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
 
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni  Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.
 
Utambulisho umeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Saluti5 na Father Kidevu Blog (www.mrokim.blogspot.com).
Posted by MROKI On Saturday, April 19, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo