Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2014

Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Jimbo la Makunduchi Zanzibar. Samia kwa sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano. 
 Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Amina Abdallah Amour. Amina ni mjumbe kutoka Visiwani Zanzibar.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wanaomuunga mkono mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan wakimsindikiza mgombea huyo kwa hoi hoi, vifijo na nderemo kurejesha fomu yake ya kuwania nafasi hiyo kwa Katibu wa Bunge mjini Dodoma leo.
 Hapa wakitaka kumbeba mgombea wao baada ya kurejesha fomu
 Wajumbe wanaomuunga mkono wakimpongeza baada ya kurejesha fomu.

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila akipokea fomu ya ugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suhu Hassan jana asabuhi kabla ya uchaguzi kufanyika jioni. Samia alikuwa akiungwa mkono na wajumbe wengi kutoka Tanzania bara na visiwani ukilinganisha na mpinzani wake Amina Abdalah Amour nae kutoka Zanzibar.
 
 Mgombea nafasi ya Makamu Mwernyekiti wa Bunge la Katiba, Amina Abdallah Amour akisindikizwa na wapambe wake kurejesha fomu.

Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Amina Abdalah Amour akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila jana asabuhi kabla ya uchaguzi kufanyika jioni. Amina alikuwa akichuana na mgombea mwenzake Samia Suluhu Hassan.
Posted by MROKI On Thursday, March 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo