Nafasi Ya Matangazo

February 06, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa rasimu ya katiba kwa viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa baada ya kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christofa Mtikila kwa kipigo, ambapo Mtikila alimweleza Rais kuwa licha ya watuhumiwa wake kufahamika lakini hawajakamatwa na Polisi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kufungua mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014 katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika chumba cha mkutano huo.


 viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakifuatilia mkutano huo.

Rais Kikwete akisalimiana na Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu 
Posted by MROKI On Thursday, February 06, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo