Nafasi Ya Matangazo

October 22, 2013

FOMU za mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinatarajiwa kuanza kutolewa kesho Jumatano, huku Watanzania wakiombwa wachangie kwa gharama ndogo.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, katika kuhakikisha kila mtu anashiriki kutakuwa na vituo 13 vitakavyofunguliwa kwa ajili ya kutoa fomu hizo, huku pia kukiwa na watu maalumu watakaozisambaza maofisini na hata majumbani.
 
Melleck alisema, fomu hizo zitatolewa kwa Sh 100,000 kwa wale watakaotaka kukimbia mbio za kilomita tatu, Sh 2,000 mbio za kilomita tano, Sh 6,000 kwa atakayeshiriki moja kati yam bio za kilomita 21 au 42.
 
“Hizi mbio ni muhimu zaidi kwa ajili ya Taifa letu, hivyo ni vyema kwa Watanzania wote wakashiriki ili kuipigania amani iliyopo nchini mwetu.
 
“Tunataka kuungana na Rais Jakaya Kikwete katika kuhakikisha tunakuwa sehemu ya kuleta umoja, amani na mshikamano ndani ya Tanzania na ndilo lengu la mbio hizi.
 
“Bado tunaendelea kuwaomba wadhamini wajitokeze kuzidhamini, kwani nafasi bado ipo wazi na watambue hata wao ni sehemu ya kupigania amani ya taifa letu,” alisema Melleck.
 
Katika mbio hizo, zitakazowashirikisha watu wa kada mbalimbali, zitakuwepo pia mbio za kilomita 3, kilomita 5, Half Marathon kilomita 21 pamoja na Full Marathon yenyewe kilomita 42.
 
Mratibu huyo anasema mbio za kilomita 3 zitakuwa maalumu kwa ajili ya viongozi wa kada mbalimbali, wakiwemo pia wale wa dini na zile za kilomita 5 pia zitakuwa za kuchangia kwa ajili ya watu wa mahitaji ya aina mbalimbali.
 
“Hapa tunachotaka kufanya katika mbio za kilomita 3 ni kuwaomba kama vile viongozi maarufu wa dini mbalimbali pamoja na viongozi wetu ili kushiriki, kwa kudumisha amani na upendo.
 
“Pia tutahakikisha kama mbio za kilomita 5, zinakuwa kwa ajili ya kuchangia watu wenye mahitaji mbalimbali na tayari tuna uhakika mkubwa wa wanariadha maarufu zaidi duniani kushiriki,” anasema.
 
Mratibu huyo anafafanua kuwa wamejipanga mno katika hilo ili kuhakikisha wanafanya mambo makubwa zaidi na ambayo yataleta tija kwa taifa.
Posted by MROKI On Tuesday, October 22, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo