Nafasi Ya Matangazo

September 23, 2013

1aKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu wakati alipomtembelea na kumjulia hali Mjini Butiama leo, wakati akiondoka wilayani humo kuelekea Mugumu Wilaya ya Serengeti kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho, Jenerali Musuguli alionekana kuwa na bashasha wakati alipomuona Abdulrahman Kinana pengine ni kutokana na utendaji kazi wa katibu mkuu huyo wa CCM, ambapo alisikika akisema huyu ni kijana wangu huku wakiwa wameshikana mikono wakiingia ndani kwa mazungumzo ya faragha. 2a 
Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu akisalimiana na Nimrod Mkono Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi CCM. 22Mwalimu Peter Simon wa shule ya Sekondari ya Nata wilayani Serengeti akielezea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wake somo la sayansi wakati alipotembelea maabara ya shule hiyo.katikati ni mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph 23a mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM kuhusu wanafunzi hao wanavyojifunza jinsi ya kutengeneza sabuni katika maabara hiyo
PICHA ZAIDI BOFYA----FULLSHANGWE BLOG
Posted by MROKI On Monday, September 23, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo