Nafasi Ya Matangazo

June 22, 2013



 Wakili Froldius Mugisha Mutungi (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakili Emmanuel Tamila Makene (wapilikushoto) pamoja na Mkewe mama Mutungi na kijana kutoka Ofisi ya Kings Low Chember, Daudi. 
*********


Ama kweli penye nia njia hupatikana….
Msemo huu wa wahenga umekamilika tarehe 21 Juni 2013 ambapo Ndugu Froldius Mugisha Mutungi ameapishwa kuwa wakili wa kujitegea.

Muuguzi huyu anamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumpa afya ya mwili, roho na akili pia. Na anawashukuru sana familia yake hasa mke wake ,wafanyakazi wenzake, ndugu jamaa na marafiki ambao wamemsaidia kwa njia moja au nyingine hata kupatikana mafanikio haya.


“Hakika ilikuwa safari ndefu iliyojaa milima na mabonde mpaka kufikia hapa nilipo. Inahitaji kuwa na malengo ,ujasiri na uthubutu, kujituma na kuwa na dhamira ya kweli ili kuyafikia malengo. Ni safari ambayo inahitaji kujitoa sadaka kwa mambo mengi kuanzia familia,ndugu jamaa, marafiki shughuli za kijamii na hata kazi. Wakati mwingine inahitaji kuweka rehani baadhi ya mambo muhimu ili kusonga mbele.

Katika safari kama hii inahitaji uwe na msimamo wa kusimamia maamuzi yako. Nilipoanza chuo mwaka 2006 pale Chuo Kikuu Huria cha Tanzania baadhi ya watu tena wengine watu wangu wa karibu walinikatisha tama lakini wapo walionitia moyo.

 Namshukuru sana mke wangu alinielewa pamoja na kwamba nilimwachia mzigo mkubwa wa kuendesha familia wakati niko shule hasa wakati nasoma shule ya sheria. Kazinin nako mambo hayakuwa rahisi lakini kwa kuwa nia nilikuwa nayo, sababu nilikuwa nazo na uwezo pia nikuwa nao nilibakiza kazi moja tu, kusoma na kufaulu.

Tangu nikiwa mdogo sikupenda kuona mtu anadhulumiwa au kunyanyaswa, nilipenda sana haki.Lakini baba yangu Mzee John Mutungi aliwahi kuniambia kuwa “haki haipatikani kirahisi na ina gharama, tena gharama kubwa kwelikweli…” Sikumelewa wakati huo alichomaanisha.

 Nilipofika kazini kama Afisa Muuguzi Msaidizi nilikuta mambo ni tofauti na nilivyotegemea.Nilitafuta njia ya kuwatetea wanyonge lakini kila mara nilikwaa visiki. Nilipotafakari sana, nadhani Mungu akaniongoza nisome sheria kwani hata nilipokwenda chuo kuchukua fomu za kujiunga sikuwa nimefikiria kusoma sheria.

Leo sasa yametimia, Mungu amejibu maombi, “ hakika ameutazama unyonge wa mjakazi wake”. Naweza sasa kuwasemea na kuwatetea wanyonge wasioweza kujisemea au kujitetea.
Posted by MROKI On Saturday, June 22, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo