Nafasi Ya Matangazo

January 18, 2013

Mwaka ulioisha hivi karibuni umeonyasha, baada ya miaka mingi, kuongezeka kwa chuki katika jamii ambayo awali ilikuwa inaishi kwa amani kati ya Waislamu na Wakristu Afrika Mashariki. Mwandishi Isaac Mwangi wa Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) anatathmini hali hiyo isiyo ya kufurahisha ya mgogoro kati ya Waislamu na Wakristu ambayo ilitia doa la mahusiano mwaka jana…Hii hapa taarifa yake.

Arusha Januari 15, 2013 (EANA) - Agosti 27, Kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu nchini Kenya, Shehe Aboud Rogo aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake mjini Mombasa.Vijana wa Kiislamu katika mji huo wa ukanda wa Pwani walianzisha ghasia mara moja baada ya tukio hilo ambapo waliharibu na kuchoma moto makanisa katika vurugu za kiimani mbaya zaidi kuwahi kutokea katika nchi Kenya. Viongozi wa dini toka pande zote mbili walijaribu kwa kila hali kuwasihi wafuasi wao na kurejesha tena utulivu katika eno hilo. 

Lakini tukio hili ni la pekee zaidi ambapo lilishuhudia uvumilivu wa dini tofauti ukiwa umejaribiwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka 2012 kwa nchi za Kenya na Tanzania.

Mapema,Jumapili ya Julai mosi,mabomu mawili yalirushwa kwa waumini waliokuwa wanasali katika makanisa mawili tofauti, enee la Garisa,katika mkoa wa Kaskazini Mashariki unaopakana na nchi ya Somalia. Jumla ya watu 17 walikufa, wakiwemo polisi wawili waliokuwa wanalinda moja ya makanisa hayo.Pia waumini 60 walijeruhiwa.

Kiongozi huyo wa Kiislamu, Shehe Rogo aliyeuawa, awali alitamka wakati wa swala ya Ijumaa msikitini mjini Mombasa kufuatia mashambulizi hayo ya Garisa kwamba tukio hilo lilifanywa na Waislamu kulipiza kisasi. Polisi hawakumkamata.
Wakati tukio hilo lilitoa ishara ya Waislamu kuishi kwa mashaka na Wakristu nchini Kenya, hali kama hiyo ya mashambulizi ya moja kwa moja haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka lukuki.


Wiki tatu baada ya mashambulio ya Garisa,polisi nao walikamata mabomu yaliyokuwa yanadaiwa kuwa yangetumika kulipua kanisa Katoliki la Assumption of Mary, katika Parokia ya Umoja, jijini Nairobi. Watu wawili waliokamatwa na mabomu hayo waliripotiwa kuwa waliyaingiza mabomu hayo kutoka nchi moja jirani na Kenya.

Kwa upande mwingine wa mgawanyiko huo kwa misingi ya kidini, kulikuwepo pia kupamba kwa uhasama miongoni mwa jamii za Waislamu wenyewe.Jarida la kila wiki linalochapishwa na Jamia Mosque mjini Nairobi la The Friday Bulletin,liliripoti Agosti kwamba waislamu wenye imani kali walibomoa msikiti mmoja katika wilaya Kajiado,kumwagia kinyesi msikini na kuchoma moto nakala za Korani, Kitabu Kitakatifu cha Waislamu. Msikiti huo ulikuwa unajengwa eneo la Olkejuado High School, ulikuwa unakaribia kukamilika.


Katika tukio la pili,Mwalimu Mkuu wa Kangeta High School, Meru aliwatimua wanafunzi 15 baada ya kusisitiza kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhani, hivyo kwenda kinyume na amri ya mkuu wao wa shule.

Kujihusisha kwa Kenya, kijeshi nchini Somalia tangu Oktoba 2011, ambako jeshi la nchi hiyo linapambana na kundi la wanamgambo la Al Shabaab lilifungulia kuliongeza kwa matukio ya kigaidi.Mashambulio hayo kwa kiasi kikubwa yalifanya hali ya uhasama kuwa mbaya zaidi 2012 kati ya dini hizo mbili kuu nchini Kenya za Kikristu na Kiislamu. 

 
Nchini Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda alitiwa mbaroni Oktoba baada ya waandamanaji wa Kiislamu kutaharuki na kuchoma makanisa matano jijini Dare es Salaam.

Ghasia hizo zilizuka baada ya mvulana wa Kikristu kudaiwa kukojolea nakala ya Korani. Zaidi ya watu 120 walitiwa mbaroni kufuatia ghasia hizo, ambazo zilijenga uhasama mkubwa kati ya Waislamu na Wakristu, katika moja ya matukio mabaya zaidi ya kidini kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania bara. 

Kulikuwapo pia ghasia katika kisiwa cha Zanzibar wakati kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu, Shehe Farid Hadi Ahmed alipotekwa asubuhi ya Oktoba 16. Kanisa la Jimbo la Christ Church lilipo eneo la Mji Mkongwe kisiwani hapo lilishambuliwa na waamini wake kuondolewa haraka ili kuwanusuru.

Uganda haikupata matukio ya migogoro mikubwa ya kidini kama ilivyokuwa kwa Kenya na Tanzania.Lakini Mwinjilisi wa kanisa la Pentekoste, ambaye aliwashawishi maelfu ya waumini ya Kiislamu kujiunga na Ukristu aliharibiwa uso wake wakati wa usiku wa Krismasi 2012, tukio ambalo lilileta hofu baina ya waumini wa dini hizo mbili pia. 

Kwa nchi za Rwanda na Burundi hapakuripotiwa matukio yoyote yasiyo ya kawaida yaliyoleta mvurugano baina ya Waislamu na Wakristu.
Posted by MROKI On Friday, January 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo