Nafasi Ya Matangazo

November 05, 2012

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkonX6xgV5R9XMOUhyphenhyphenASeTt08-FsoF5wE6o9y8D3i_BAoKiJU-SMBSQVXPu5TIIBQ5OtE7GluEhhQKbR0WFzq-EB8K5PF2sylwiB1VXIRPoOC6Cbvsvsd31y0DEi-TKZQP0BuomI39fWnC/s1600/balozi.jpg
Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Amour Zacarias Kupela (kulia) Picha maktaba

Aliyekuwa Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Bw.Amour Zacarias Kupela amekabidhi msaada wa vifaa vya Kusomea vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.2 kwa wanafunzi 500 wa Shule ya sekondari masonya zikiwa ni juhudi za nchi yake kudumisha urafiki na Tanzania.

Msaada huo uliotolewa na kiongozi huyo  ni madaftari makubwa (Counter Book 500), Peni 500 na Pensel 500 na Mipira 5 umetolewa kutokana na mapenzi ya Balozi huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kuenzi kumbu kumbu za wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na eneo ambapo ilianzishwa Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Msumbiji (OMM) march 16/1973. 

Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Balozi Kupela  katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania Bw.Daniel Rui Simao Ntada alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa ahadi ya Balozi huyo aliyo itoa wakati alipofanya ziara ya kuaga viongozi wa Wilaya ya Tunduru ambapo aliahidi kuisaidia Shule hiyo iliyopo katika eneo la kambi ya wapigania uhuru wa Chama Cha Frelimo Nchini Msumbiji .

Akifafanua taarifa hiyo Bw. Rui alisema kuwa Balozi Kupela alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea katika eneo hilo muhimu kwa historyia ya wapigania uhuru wa Nchi yao ambapo palikuwa ni miongoni mwa kambi kubwa za wapigania uhuru wa nchi yao wakiwemo Kamarada Samora Machel, Marcelino Dos Santos, Rais wa sasa Armando Guebuza, Dkt. Edward Mondlane na wengine wengi.

Katika taarifa hiyo pia Bw. Rui kwa niaba ya Balozi Kupela alisema Msaada huo ni juhudi za Balozi huyo kuendeleza kudumisha urafiki wa nchi hizo pamoja na kutunza, kuyahifadhi maeneo yote ya kumbu kumbu na kuenzi historia ya Tanzania na Msumbiji.

Bw. Rui alibainisha kuwa Kwavile Chama cha Frelimo Kilianzishwa Tanzania kwa kutoa baadhi ya maeneo ya ardhi yake kwa Chama hicho Cha Frelimo ambapo wapigania Uhuru hao walijenga Kambi za Kijeshi katika maeneo ya Nachingwea,Kongwa,Bagamoyo,Masonya na katika Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara ili wapigania uhuru  waendelee kutibiwa .

Mwl. Ngaunje katika hotuba yake pia alipokea mwaliko wa kupeleka Wanafunzi wa Shule yake katika Ziara ya kubadilishana taaluma katika Shule ya Sekondari Mekula iliyopo  Mkoa wa Niasa Nchini Msumbiji

Wasemaji wengine katika hafla hiyo walikuwa ni Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila mwakilishi wa Afisa elimu Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Kerlen Kitosi ambao pamoja na kumpongeza Balozi Kupela kwa msaada huo pia walipongeza juhudi zake za kuendeleza elimu ya Tanzania.
 SOURCE: DEMASHONEWS BLOG
Posted by MROKI On Monday, November 05, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo