Nafasi Ya Matangazo

July 28, 2012

Magoli mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo fainali.

Yanga pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.
Posted by MROKI On Saturday, July 28, 2012 1 comment

1 comment:

  1. Ongeza kwamba Yanga wanachukua kombe hili kwa mara ya pili mfululizo halafu ondoa maneno ya kulipa kisasi kwa Azam.... maana kisasi tutalipa ktk ligi kuu na sio huku ambako Azam ndo wamecheza kwa mara ya kwanza kaka

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo