Nafasi Ya Matangazo

July 03, 2012

 Meneja uhusiano Mwandamizi wa Benki ya Posta NovesMoses (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya huduma za Benki hiyopopote(TPB Popote) ambapo mteja anaweza kutoa na kuweka pesa zake popote alipo. Meneja huyo alitoa maelezo hayo leo jijini Dar es salaam kwenye banda laWizara ya Fedha wakati wa maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar essalaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere.
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Akiba wa wafanyakaziserikalini (GEPF) Deogratius Urio (kulia) akisikiliza maswali mbalimbali  kutoka kwa Askari Polisi jana jijini Dar essalaam waliotaka kujua faida za kujiunga na Mfuko wakati walipotembelea bandala Wizara ya Fedha  kwenye  maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere.
 Waziri mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo chaUsimamizi wa Fedha(IFM) Sarungi Daniel (kulia) akimwelekeza mwananchi juu yataratibu ya kujiunga cha IMF katika kozi mbalimbali jana jijini Dar es salaamwakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonyeshoya 36 ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.
 Afisa Habari na Mawasiliano wa Mfuko wa Changamotoza Melenia Tanzania (MCAT) Josephat Kinyunyu (kushoto) akitoa maelezo kwawananchi leo jijini Dar es salaam kuhusu miradi mbalimbali inayosimamiwa namfuko huo wakati wananchi hao walipotembelea banda la Wizara ya Fedha  kwenye maonesho ya 36 ya biashara ya kimataifa ya Dar es salaam yanayoendeleakatika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere.
 Afisa Manunuzi kutoka Dhamana ya UwekezajiTanzania(UTT) Hamis Kiimbi (kulia) akimwelekeza mwananchi juu ya taratibu ya kuwekezakatika mfuko huu jana jijini Dar es salaam wakati mwananchi huyo alipotembeleabanda la Wizara ya Fedha katika Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya Dar es salaamyanayoendelea.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda laWizara ya Fedha kwa upande wa Chuo cha Mipango wakiandika maoni yao jana jijiniDar es salaam mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonyesho ya 36 yaKimataifa ya Dar es salaam yanayoendelea.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha wakitoahuduma jana jijini Dar es salaam kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya 36 yaKimaifa ya biashara ya Dar es salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, July 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo