Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka Ngao na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Kutoka (kushoto) Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo Julai 25, 2012
Posted by MROKI On Wednesday, July 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo