Nafasi Ya Matangazo

July 27, 2012

Lady Jay Dee akiimba kwa msisitizo kabisa mbele ya wageni (hawapo pichani)  waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana sana,ambayo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali katika Hoteli ya Mount Meru jiji Arusha wakati wa hafla fupi ya kusherekea kwa uzinduzi wa Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.
Mmoja wa wasanii mahiri kutoka kituo cha wenye vipaji cha THT,Barnabas sambamba na bendi yake kwa pamoja wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya uzinduzi rasmi wa kusherekea kwa uzinduzi wa Shirika la ndege la serikali ya Qatar (Qatar airways) huduma ya safari zake za anga kutoka Kilimanjaro kuelekea sehemu mbalimbali za dunia kila siku na kufanya huduma za safari za anga kufikia zaidi miji 118.Tafrija hiyo ilifunguliwa rasmi na mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe.
Barnaba akiimba huku akipiga kitaa kuonesha kipaji chake alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana sana,ambayo ilihudhuria na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali.
 Sehemu ya Meza ikifurahi jambo kwa pamoja.
 Sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
 Wadau kutoka Ughaibuni nao walikuwepo kwenye mnuso wa hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe,kama aonekavyo pichani,Dr Mwakyembe alieleza kuwa Mwakyembe amesema kuwa serikali ina mpango wa kuboresha viwanja vya ndege hapa nchini ili kuweza kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa kwa ujumla,alisema kuwa katika bajeti ambayo itawasilishwa mwezi ujao suala la kuboresha viwanja vya ndege vya Nchi nzima litapewa kipaumbe hivyo kuifanya nchi kukua kiuchumi zaidi.
 Pichani kati ni waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akibadilishana mawazo na wadau wengine kwenye hafla hiyo.
waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe (pichani kati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar wakiwasili kwenye hafla hiyo.
Wadua Gadna G Habash pamoja na Charlz Muhamiji a.k.a Mr C nao walijumuika kwa pamoja kwenye mnuso huo uliofana kwa kiasi kikubwa.
Posted by MROKI On Friday, July 27, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo