Nafasi Ya Matangazo

June 06, 2012

Meneja wa bia ya Serengeti Bw. Allan Chonjo (wa pili kushoto) akichezesha droo ya sita ya promosheni ya Vumbua hazina chini ya kizibo na SBL, inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar leo. Kulia ni James Ndetiko kutoka PWC na Bakari Magged Kutoka bodi ya bahati nasibu ya Taifa, kushoto ni Tumainieli Malisa kutoka  PWC pamoja na waandshi wa habari na wadau wengine wakifuatilia kwa ukaribu Droo hiyo.Katika droo hiyo iliyochezeshwa leo, Deusdedit Njau (22) ambaye ni mkazi wa Kiboroloni mjini Moshi mkoani kilimanjarro amejishindia jenereta mpya na  mshindi mwingine ni Vicent Lymo (36) kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro amejishindia bajaji.
**********
Kampuni ya bia ya Serengeti leo imeendelea na droo ya sita ya promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa wikya sita sasa ambapo katika droo hiyo washindi wawili walipatikana ambao ni bw. Deusdedit Tobias Njau 22 kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosh mkoani Kilimanjaro ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kabisa.

Droo hiyo ilichezeshwa asubuhi ya jana katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti SBL zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE, wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Akiongea na waandishin wa habari wakati wa kutangaza washindi wa droo hiyo, Meneja wa bia ya Serengeti bw. Allan Chonjo amesema washindi hao watakabidhiwa zawadi zao siku chache zijazo na kwamba washindi wa droo iliopita watakabidhiwa zawadi zao leo jioni huko Kilimanjaro  na wiki mwishoni mwa wiki hii washindi wengine waliopatikana huko mwanza watakabidhiwa zawadi zao “ kwasasa kinachofanyika sasahivi ni taratibu za usajili na usafirshwaji kwa wale washindi wetu wa mbali kwani sisi tunamfuata mshindi wetu popote alipo. Alisema bwana Chonjo.

Bw. Chonjo aliwapongeza washindi wote katika droo hiyo na kuwataka watanzania waendelee kunywa bia za Serengeti ambazo zimeainishwa katika promosheni hiyo ili kuendelea kushinda na hatimaye kupiga hatua katika maisha yao.

Hii ni droo ya sita wiki ya sita mfululizo ambapo bado takriban wiki kumis sasa ili kuisha kwa promosheni hiyo ya pekee na aya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni 780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini
Posted by MROKI On Wednesday, June 06, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo