Nafasi Ya Matangazo

June 20, 2012


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima zake za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Willy Edward ambaye alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jambo Leo aliefariki ghafla huko mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.Hafla hii ya kuaga imefanyika mchana huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa watu waliofika kuuaga Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Juni 20.2012 kabla ya kuusafirisha kwenda Mugumu Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara kwa Maziko. Marehemu Willy alifariki usiku wa kuamkia Jumapili, Juni 17, 2012  mjini Morogoro alikokuwa amekwenda kikazi.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika majonzi.


Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd,  Dk. Reginald Mengi (kulia), akijadiliana jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye (katikati) na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),  Prof. Ibrahim Lipumba.

Mwili wa Willy Edward ukiwasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd,  Dk. Reginald Mengi akitoa salamu za pole.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akitoa salamu za pole.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye akitoa salamu za pole kutoka Chama cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda akitoa salamu za pole.

Mpiganaji Athuman Hamis akiuaga mwili wa marehemu. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Jambo Concept, Juma Pinto ambaye ndiye aliyekuwa mwajiri wa marehemu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnaye akitoa heshima za mwisho wa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF),  Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima za mwisho wa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akitoa heshima za mwisho.

Umati ukisubiri kuuaga mwili wa marehemu Willy.

Mjane wa marehemu, Rehema (kushoto), na watoto wake wakiwa katika  majonzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Marehemu Willy Edward Ogunde.
Mwandishi wa Habari, Asha Kigundula akilia kwa uchungu huku akitulizwa na waandishi wenzake, baada ya kuuaga mwili wa Marehemu Willy Edward Ogunde. Kulia ni Somoe Ng'itu wa Nipashe.


Hali ilikua tete watu wengi walipoteza fahamu wakati wa kuuaga mwili.



Niacheni... niacheni... niacheni nimshike kwa mara ya mwisho... niacheeeeni nimshike Willy... jamani Willyyyy........... hivyo ndivyo mambo yalivyojiri.

Wahariri wakipakia jeneza lenye mwili wa Willy Edward Ogunde tayari kwa safari ya Mugumu.

Hapa ukitolewa tayari kwenda kupakia kwenye gari.SOURCE:DAILY MITIKASI BLOG
Posted by MROKI On Wednesday, June 20, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo