Nafasi Ya Matangazo

May 25, 2012

Kutoka kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania,Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin,Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar,Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania,Rais Thambo Mbeki wa Afrika Kusini,Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria,Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania na Rais Rupiah Banda wa Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mchana kabla ya kuanza mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

************
Marais Wastaafu nane wa nchi za Afrika wamekutana leo jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kufanya mkutano wa siku tatu ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand. Ajenda kuu ya mkutano huo ni kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika.

Marais wastaafu hao waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Rais Ali Hassan Mwinyi wa Tanzania, Rais Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin, Rais Pedro Pires wa Cape Verde, Rais Benjamin Mkapa wa Tanzania, Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar na Rais Rupiah Banda wa Zambia.

Aidha - mbali ya Marais hao waliohudhuria mkutano huo, pia ulihudhuriwa na  Wataalam mbalimbali wa nishati, viongozi wa umma na sekta binafsi na wanafunzi na kitivo kutoka vyuo vikuu 9 vya kimataifa kikiwemo chuo kikuuu mwenyeji cha Witwatersrand a.k.a Wits. Tanzania iliwakilishwa na wanafunzi watano na walimu wawili kutoka chuo kikuu cha Dar-es-Salaam.

Mratibu mkuu wa mkutano huo - Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kujadiliana juu ya ufumbuzi wa mageuzi ya nishati katika nchi za Kiafrika, na kuhakikisha nchi za Afrika zinajiwakilisha vyema katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika suala zima la Nishati. Balozi Stith alisema kuwa mkutano huo utaleta mshikamano wa pamoja kwa viongozi wa sekta ya nishati na wafadhili mbalimbali wa miradi mbalimbali, ili kuhakikisha nishati hiyo inatosheleza mahitaji ya Afrika kwa ujumla.Mkutano huo wa siku 3 utafikia tamati Mei 25.
Posted by MROKI On Friday, May 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo