Nafasi Ya Matangazo

April 01, 2012

YAH: KUWATANGAZIA WADAU KUHUSU “PUBLIC HEARING” JUMATATU TAREHE 02 APRILI, 2012

Ofisi ya Bunge kupitia Kamati yake ya Viwanda na Biashara inaendelea kutekeleza majukumu yake katika kipindi hiki cha Mikutano ya Kamati za Bunge inayoendelea katika Ofisi ndogo za Bunge, Dar es Salaam. Hii ni kwa mujibu wa Kanunui za Kudumu za Bunge, Nyongeza ya Nane (9) (1) Toleo la 2007.

Mojawapo ya shughuli zinazofanyika wakati wa Vikao hivi na kamati hii ni kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Biashara (The Business Laws (Miscellaneous Amendments) ACT, 2011
unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni katika Mkutano ujao. Ili kukidhi masharti ya Kanuni ya 84(2), ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2007, Kamati imepanga kusikiliza na kupokea Maoni ya Wadau katika Muswada huu (Public Hearing) tarehe 02/04/2012 kuanzia saa 3 Asubuhi, katika Ukumbi wa  Karimjee, Jijini Dar es
Salaam.

Wadau wote wanakaribishwa kuja kushiriki kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha Muswada huu kabla ya kupita katika hatua zake zote na kuwa sheria kamili baada ya kupitishwa na Bunge.

Wadau wote watakao sikia mwaliko huu kupitia vyombo vya Habari, wawaarifu na wengine kwa lengo la kuja kutoa maoni yao ili kuboresha Muswada huu wa Marekebisho ya Sheria za Biashara (The Business Laws (Miscellaneous Amendments) ACT, 2011.
Imetolewa na 
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi za Bunge
Dar es Salaam
31 Machi, 2012
Posted by MROKI On Sunday, April 01, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo