Nafasi Ya Matangazo

August 28, 2011

Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad saul,  wakiwa pamoja wakati wakisubiri muda wa swala kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam jana Agosti 27.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Dadick, wakiomba dua kwa pamoja baada ya kupata futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake Oysterbay jijini jana, Agosti 27,2011.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, baada ya hafla ya futari.
Rais Dkt. Jakaya kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiagana na baadhi ya wananchi waliofika katika futari iliyoandaliwa na mwenyeji wao Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais , Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya CXC Africa Ltd, Charles Hamkah.
Posted by MROKI On Sunday, August 28, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo