Nafasi Ya Matangazo

March 29, 2011

 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza  wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.
 Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia  mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa  wakati wa  mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, March 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo