Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2010

TANZIA Marehemu Redemptus a.k.a TEMBE
Uongozi wa Kampuni ya MEDIA SOLUTIONS LTD wachapishaji wa magazeti ya ThisDay na KuliKoni unasikitika kuwatangazia kifo cha ghafla cha mfanyakazi wake, Redemptus Angelo (pichani) wa Kitengo cha Usanifu Kurasa (Chief Graphic Designer)

kulichotokea Jumapili Agosti 01, 2010 Saa 4.00 usiku katika Hospitali ya Mwananyamala.

Taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Marehemu TEMBE aliwahi pia kufanya kazi IPP MEDIA katikaMagazeti ya The Guardian LTD na MWANANCHI COMMUNICATIONS LTD.
Posted by MROKI On Monday, August 02, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Naipa pole sana familia ya RAFIKI yangu, NDUGU yangu KAKA yangu na MFANYAKAZI MWENZANGU Redemptus Angelo. Tukiwa Mwananchi communications limited tulifahamiana vizuri na REDE. Alikuwa mtu mwema sana, wengi wataniunga mkono. Alikuwa hana makuu. Binafsi nimeguswa sana na msiba huu. Mara ya mwisho nilimpigia simu niliposhuka posta mpya nikielekea nyumbani mbagala kutoka kazini the guardian ltd. katika kupokea simu alikuwa na kawaida ya kucheka sana nikimpigia, alicheka sana na kuniuliza uko wapi wewe msukuma wa mbagala. nikamjibu niko posta mpya naelekea nyumbani, lakini usafiri wa shida nimeamua kupumzika mjini niangalie world cup kidogo. "nimekupigia unionyeshe kijiwe kizuri cha kucheki ball" nilimwambia, na kunijibu "njoo ofisini nikupeleke". Basi nilienda na tukatoka naye. ukweli tuliangalia mechi na baada ya mechi tulifurahia kuwa marafiki kwa kula nyama na bia kidogo. Nasikitika sana nimempoteza rafiki wa kweli. Mwenyezi mungu ailaze roho yake mahala PEMA PEPONI, Amin Mimi ni KITEJA NTOBELA MAYUNGA.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo