Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2010

Mwenge huo mwenge!!!tunaukimbiza mbiombio...hadimakaoo makuu...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2010 katika Uwanja wa Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2010 katika Uwanja wa Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara leo, tayari kwa ajili ya kukimbizwa katika Mikoa yote ya Tanzania. Wa pili Kushoto Waziri wa Kazi Vijana na Ajira Mhe. Juma Kapuya na Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana na Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Asha Abdalla Juma. Ujumbe wa Mwenge mwaka huu ni tokomeza malaria, ugonjwa wa ukimwi na mauaji ya Albino.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akianzisha harakati za kukimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2010, mara baada ya kuuwasha rasmi katika Uwanja wa Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara leo. Kulia Waziri wa Kazi Ajira na Vijana Maendeleo ya wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Asha Abdalla Juma.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2010 Nassoro Ally Matuzya kutoka Mkoa wa Dar es salaam tayari kwa ajili ya kukimwizwa katika Mikoa yote ya Tanzania.

Posted by MROKI On Saturday, May 29, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo