Nafasi Ya Matangazo

May 29, 2010

Wazazi na watoto wakisubiri foleni ya kuchukua vyandarua vyao leo.
Wengine waliamua kukaa chini kusubiri foleni.
Mkazi wa Mazizini Ukonga, Dar es Salaam akisaini ili kupata chandarua kwaajili ya mtoto wake.
Mtoto akiwa amebeba Chandarua alicho gawiwa jana katika zoezi linaloendelea.
Mtoto akisubiri mgawaji Musa Komba kusoma namba ya kadi.
Mtoto Isdori Didas akiwa na chandarua chake.
Baadhi ya wazazi walilalamikia namna zoezi hilo linavyo enndeshwa katika ofisi hiyo ya Serikali za Mtaa Mazizini Kata ya Ukonga, Dar es Salaam ambapo jana waliambiwa kuwa zoezi lingeanza saa 10 jioni lakini likaanza saa 2 asubuhi kwa kile viongozi wa Mtaa huo kudai kuwa hawakuwa wakijua hasa zoezi lianze saa ngapi.
Aidha Mwenyekiti wa Mtaa huo Joseph Kabati alisema zoezi linaenda vizuri lakini watu wengi wa mtaa wake wamekuwa wakifika ofisini hapo kulalamika kuwa hawakuandikishwa jambo ambalo linawafanya wakose vyandarua hivyo.
Pia watoto walio na umri wa miaka 5 hawapewi vyandarua hivyo kwa kile viongozi hao walichodai kuwa wanao stahili ni wale wenye mwaka 0-4 na miezi 12 (kwa tafsiri ya miaka chini ya 5) jambo ambalo baadhi ya wazazi wamelilamikia.
Posted by MROKI On Saturday, May 29, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo