Nafasi Ya Matangazo

March 30, 2010

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela (wapili kulia) akipeana mkono na Meneja wa Bia ya Kilimnanjaro George Kavishe (kushoto) huku Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja na Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijake (kulia) wakishuhuda baad aya kuzinduliwa kwa ligi ya taifa yatakayofanyika Mwezi Mei kwa kushirikisha timu za mpira wa miguu mikoa yote.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Frederick Mwakalebela (wapili kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja huku Meneja wa Bia ya Kilimnanjaro George Kavishe (kushoto) na Afisa Habari wa TFF, Florian Kaijake (kulia) wakishuhuda baad aya kuzinduliwa kwa ligi ya taifa yatakayofanyika Mwezi Mei kwa kushirikisha timu za mpira wa miguu mikoa yote.
KILI TAIFA CUP 2010 LAZINDULIWA RASMI

Dar es Salaam Machi 30, 2010: Mashindano ya Kombe la Taifa (Kili Taifa Cup 2010) yamezinduliwa rasmi leo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wafanyakazi wa TBL na waandishi wa habari wakishuhudia.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Kilimanjaro Premium Lager, moja ya aina za bia za TBL kudhamini mashindano hayo yanayosaidia kung’amua na kukuza vipaji mbalimbali kuanzia ngazi za chini hadi timu ya taifa na kwenye klabu kubwa za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi. Hata hivyo ni mara ya nne kwa kampuni ya TBL kudhamini mashindano haya.

“Tunajivunia kufadhili mashindano makubwa kama haya ambayo si tu yataleta shamrashamra miongoni mwa washabiki wa soka kote nchini, lakini pia yatasaidia kung’amua vipaji vipya na labda kuwaingiza baadhi ya wachezaji hao kwenye timu za taifa au kwenye klabu zinazoongoza,” anasema David Minja, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL.

Alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yanafanyika chini ya dhima: ‘Kufikisha Soka ya Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,’ yatajumuisha timu 24 zitakazocheza katika vituo sita, ambapo inatarajiwa kwamba mashindano hayo yataanza Mei 8, 2010 hadi Mei 15, 2010 katika vituo vyote hivyo, ambapo kila timu itacheza na mwenzake kwenye ngazi za mzunguko kisha zitakazopata pointi nyingi zaidi zitaingia kwenye hatua ya robo fainali.

Kwa mujibu wa Minja, robo fainali hizo zitachezwa Mei 22, 2010 na fainali zitakuwa Mei 30, 2010, na kwamba vituo hivyo sita ni pamoja na Mtwara, Arusha, Dodoma, Tanga, Iringa na Shinyanga.

“Ufadhili kwa mashindano yote ni Tsh milioni 850 na kila timu itapokea fedha za maandalizi, usafiri na malazi pamoja na seti za sare za michezo kwa ajili ya mashindano hayo,” alisema Mkurugenzi huyo wa TBL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema; “Tuna furaha kwa kuwa mashindano ya mwaka huu pia yatahusisha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 lakini watakaocheza ni wale waliozidi miaka 18. Timu zote zimejiandaa kwa ajili ya mashindano haya, hivyo tunawaomba Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kuunga mkono timu zao.”

Kwa muda mrefu TBL imekuwa ikijifungamanisha na Kabumbu na kwa hakika inafurahia hali ya uhuishwaji wa ufadhili katika Soka.


Kwa taarifa zaidi:

George Kavishe, TBL, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, +255 767 266786, george.kavishe@tz.sabmiller.com

Michael Mukunza, Executive Solutions Limited, +255 784 978302, m.mukunza@executivesolutions.co.tz



Kuhusu TBL


Tanzania Breweries Limited (TBL) huzalisha, kuuza na kusambaza bia safi, vinywaji vyenye kilevi na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL ina maslahi ndani ya Tanzania Distilleries Limited, na kampuni zinazohusiana nayo, Mountainside Farms Limited.

Bia za TBL zenye umaarufu zaidi ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt na Castle Lager. Vinywaji vya aina nyingine vinavyohusiana na kundi la TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds na Premium Cold.

Kundi la TBL limeorodheshwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) na imeajiri karibu watu 1,300 na inawakilishwa kote nchini na viwanda vitatu vya bia, distillery, a maltings facility na depo nane za usambazaji.
Posted by MROKI On Tuesday, March 30, 2010 2 comments

2 comments:

  1. ANGALIA AFYA ZA HAO MABWANA WA TFF LINGANISHA NA WA TBL UTAPATA JAWABU KWANINI VYEO TFF WATU HUFIKA KULOGANA ,PIA ACCOUNT YA TFF SIKU ZOTE HAINA HELA MAANDALIZI YA TIMU ZA TAIFA WANAANZA TEMBEZA KAPU HIV KUNA AUDITING YA HII UDHAMINI NA MICHANGO MENGINE.

    ReplyDelete
  2. Afya ya Mwakelebela imenistua na sikutambua mpaka niliposoma na kuona jina! TFF kwa kweli kunono.. Hamna football bongo! Huyo Kaijage naye anafuata nyayo hizo hizo.. Ndo maana wanagombania sana kuingia humo!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo