Nafasi Ya Matangazo

March 25, 2010

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Shy-Rose Bhanji akipeana mkono na Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Namtumbo Paulo Gailanga baada ya kukabidhi msaada wa madawati wa madarasa mawili katika shule ya Msingi Nambehe iliyopo kijiji cha Msindo. NMB pia ilitoa misaada mbalimbali wilayani Namtumbo yenye thamani ya shillingi Millioni 10.Maafisa wa benki ya NMB wakimpa pole mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Namtumbo, wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma. Maafisa wa NMB walikabidhi magodoro na drandarua kwenye kituo hicho ikiwa ni msaada wa benki hiyo juzi. NMB pia ilitoa misaada mbalimbali kwa ujenzi wa mashule wilayani humo yote ikiwa na thamani ya shillingi millioni 10m/-. Makabidhiano hayo yalifanyikia wilayani namtumbo juzi.
Posted by MROKI On Thursday, March 25, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo