Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2010

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein wa pili kulia, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha kulia, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour katikati, na Rais mstaafu wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi, wakisoma Hitima maalum ya kuwaombea Wazee mbalimbali waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika jana katika msikiti wa kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein kulia, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa pili kushoto, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Pembe Juma katikati, Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Ali Hassan Mwinyi, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakisoma Dua ya pamoja kwenye eneo la Makaburi ya Wazee baada ya kumaliza kusoma Hitima maalum iliyoambatana na Maulid yanayosomwa kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Uguja
Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour , Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Pembe Juma, wakielekea kwenye eneo la Makaburi ya Wazee walitangulia mbele ya Haki mara baada ya kusoma Hitima maalum kwa ajili ya Marehemu hao katika Msikiti Mkuu wa kijiji cha Kidombo uliopo Mkoa wa Kaskazini Unguja jana. Dua hiyo iliambatana na Maulidi ya nayayosomwa kila mwaka kijijini hapo.Makamu wa Rais wa Dk. Ali Mohamed Shein (wapili kulia), Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk. Salimin Amour wa (wapili kushoto) na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, wakisoma Dua ya pamoja baada ya kumalizika Maulid ilioyoandaliwa na Dk. Salimin Amour, inayofanyika kila mwaka katika kijiji cha Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Posted by MROKI On Sunday, March 07, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo