Nafasi Ya Matangazo

March 18, 2010

Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica- Elyston Angai(kulia) Pasia Budansi(kati) na Jadol Fidifosi FFU- wakitumbuiza katika ukumbi huo.
Gari la ABIRIA la Kampuni ya Mamaa Sakina Trans- likiwa kazini Posta MWENGE, Mmiliki wa magari haya na gari ndoko za Taxi jijini Dar es Salaam ndiye mwenye Mashujaa Band kitovu kipya cha Burudani.


MASHUJAA SUNDAY BONANZA -MAGEREZA UKONGA

Tunapenda kuyatambulisha kwako mashindano ya mpira wa miguu kwa kila jumapili yatakayokuwa yanafanyika katika viwanja vya Ukonga Magereza kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa nane na baada ya hapo ni burudani ya muziki wa dansi utakaokuwa unaporomoshwa na bendi mpya kabisa inayomilikiwa na kampuni ya Mashujaa Investment group iitwayo mashujaa Band ikiwa na wanamuziki wazoefu na kipaji cha hali ya juu wakiongozwa naElyston Angai.

Bendi hii inapambwa na akina dada 9 watakaokuwa wanakuletea shoo ya nguvu mara baada ya kumalizika kwa burudani ya mpira.

kampuni imeamua kuandaa mashindano hay yatakayojulikana kwa jina la MASHUJAA SUNDAY BONANZA ikiwa na lengo la kuwakutanisha wachezaji wote wa zamani na wa saa ikiwa ni kudumisha mshikamano, upendo katika jamii yetu.

Mashindano haya yatakuwa yanashirikisha timu 9 kwa kila jumapili ambapo atakuwa anatafutwa mshindi atakayekuiwa anazawadiwa mbuzi, na kila timu itakayoshiriki itakuwa inapatiwa Cret/ Catton moja moja kila moja, Bia na Maji, na pia zawadi mbalimbali zitakuwa zikitolewa kwa wachezaji -mfungaji bora, mchezaji bora na timu yenye nidhamu N.K

Mashindano haya yanaanza jumapili ya tarehe 21/03/2010 na kila timu itakuwa inatumiwa mwaliko wakati ukifika.

Kampuni inapenda kumtambulisha kwenu SPEAR MBWEMBWE (0712013093, 0754036713,0786787820.) kuwa ndiye atakayekuwa mratibu wa mashindano hayo.

Timu zinazocheza jumapili hii ni Segerea Veterani, Kipunguni Veterani, Mabibo Veterani, Fitness Fc ya Chang'ombe, Mashujaa Veterani, Mikocheni Veterani, na michezo yote itaanza saa mbili asubuhi hadi saa tisa mchana, ambapo utaratibu utakuwa Awali timu zitacheza mzunguko katika makundi mawili na washindi wa kwanza na wa pili kila kundi watavuka hatua ya Nusu Fainali ambapo timu nne zitakutana, mshindi wa kwanza kundi A atapambana na Mshindi wa Pili kundi na wa kwanza kundi B atacheza na mshindi wa Pili kundi A.

Viburudisho katika Bonanza hilo vitakuwapo, ikiwa ni pamoja na Muziki Mororo wakati michezo ikiendelea, timu zinatakiwa kufika mapema.
Mratibu wa Mashujaa Sunday Bonanza- Spia Mbwembwe.
Posted by MROKI On Thursday, March 18, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo