Nafasi Ya Matangazo

November 14, 2009

JK hapa mh! Uzalendo umepita kiasi Rais Jayaka Kikwete akikagua nyumba za wakzi wa Kijiji cha Msoga Wilayani Bagamoyo ambazo zimeharibiwa na mvua.

Ama kwa hakika ule usemi unasema "Mtu kwao na asiye na Kwao mtumwa" umedhihirika jana wakati Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara ya kukagua Nyumba kadhaa zilizoezuliwa mapaa na kuharibika vibaya katika kijiji cha Msoga Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Kitendo hicho, hakika ni cha kizalendo na kinataka moyo wa ujasiri kukifanya hasa katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika msiba mkubwa.

Ndio msiba mkubwa, kwani hujui kile kilicho tokea Jumatano iliyopita katika kitongoji cha Manka, Kijiji cha Goha Kata ya Mwamba Myamba Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.
Unakijua ila tu unataka kuntia ushahidi katika kesi yako.

Roho za watu 25 wanakadiriwa kupoteza maisha katika janga hilo kubwa kuwahi kutokea katika historia ya milima ya upareni na nchini.

Kwa maafa hayo ambayo yamepoteza si tu WAPIGA KURA bali waitikiaji wa wito na kauli mbiu ya taifa ya KILIMO KWANZA ambao ni uti wa mgongo wa taifa hili kutoka kijiji Goha.

Rais nakupongeza sana kwa kutembelea kijijini kwao na huku kwa Anne Kilango Malecela atafika yeye na DC wake Ibrahim Marwa pamoja na Mkuu wao wa Mkoa Monica Mbega.

Ninakubali kuwa hata kuezuliwa mapaa na kuharibika kwa nyumba za 'mbavu za mbwa' napo ni maafa lakini huku kwa wenzetu ni Janga kubwa maana roho za wapiga kura wenu zimetoka.

Watu wale ni juzi tu Mbunge wao aliendesha harambee ya kujenga kiwanda cha Tangawizi katika Kata yao ya Mamba Myamba, lakini sasa wakulima ndo hao wametoweka.

Mimi ni miongoni mwa watu wachache kutoka jijini Dar es Salaam ambao tumepata bahati ya kufika Kijiji cha Goha na kujionea athari hizo za maporomoko ambayo mimi naamini sio mafuriko bali kuna tetemeko dogo la ardhi lilitokea na si vinginevyo, mtaaona ripoti ya wataam wa miamba.

Mimi kwa mtazamo wangu ambao sizani kama wewe unaamini hivyo kuwa Rais Jakaya Kikwete ungeanza kwenda kuwapa pole wana Goha kwanza halafu ukarudi hapo Bagamoyo ingenipa heshima kuwa Rais wetu anatujali kwa dhiki, shida na furaha.

Huo ni mtazamo wangu tu lakini sio ukweli wa jambo lenyewe, na wala sikulazimisi kuamini kuwa JK angeanza kule ingekuwa vyema zaidi.

Lakini sio Rais peke yake hata viongozi wake wengine kama Waziri Mkuu ambaye maafa yanatokea siku kadhaa mbele huyoo anatimkia katika ziaara ya huko Lindi.

Mzee wetu Pinda kwani kulikuwa na tatizo gani kama ungefika Goha uone machozi ya wapiga kura wa Rais na Anne Kilango walivyo teketea? Naimani hata Mungu angeongeza baraka, kwani wewe Idara ya Maafa si ipo kwako?.

Ah! unaguna nini bwana kuwa sina point kwani uongo kuwa Wanagoha ni wapiga kura wa Rais na Mbunge wao Anne Kilango, Pinda wewe utaomba kura Same yanini wakati unazako huko Ruvuma.

Makamu wa Rais nawe si vibaya ukaliona hili maana wenzako wote wamezungunga muashoki na kuwaacha wapiga kura na watekelezaji wa Kilimo kwanza wameshika tama.

Jakaya sasa ni wakati muafaka kwenda Goha kuwapa pole wanakijiji maana familia nyingi zimekufa zote, na kuwapa moyo kuwa kesho ipo utarekebisha kosa la jana.

Na Huko Dodoma pia maafa yametokea yafaa twende tukawape pole sio Msoga tu nilipo zaliwa.

Nalia na wewe hadi kieleweke!

Posted by MROKI On Saturday, November 14, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo