WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amekutana na Watanzania waishio Uingereza na maeneo jirani (Diaspora) na kuwaelezea juhudi zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika sekta mbalimbali.
Mazungumzo hayo yaliwajumuisha Watanzania kutoka vikundi vya TZ-UK, ATUK, Zanzibar Welfare Association in the UK na Tanzania – UK Business Group ambavyo vinajumuisha wanachama kutoka maeneo mbalimbali ya Uingereza.
Akizungumza na Watanzania hao wapatao 350, kwenye kikao kilichofanyika jana jioni (Jumapili, Oktoba 11, 2026) katika hoteli ya Marble Arch jijini London, Uingereza, Dkt. Mwigulu aliwaeleza mipango ya Serikali ya kuboresha miundombinu na hasa usafiri wa reli, ujenzi wa bomba la mafuta, maboresho ya sekta ya elimu, maji, umeme na kilimo.
“Hali ya uchumi nchini Tanzania imezidi kuimarika licha ya kwamba nchi yetu ilipitia kwenye changamoto ya UVIKO-19, mabadiliko ya sera za biashara duniani na migogoro na kivita katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mashariki ya Kati, uhaba wa fedha za kigeni na mafuriko ya kule Hanang,” alisema.
Kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), Waziri Mkuu alisema Serikali imekamilisha ujenzi wa reli hiyo kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma na kwamba wakandarasi wako site katika vipande vyote hadi kile cha kutoka Kigoma kwenda Musongati, Burundi.
“Kutoka Isaka hadi Mwanza tumekaribia kumaliza. Sasa tunakazania kipande cha Isaka Tabora na Isaka hadi Manyoni ilii tuunge na sehemu ya Makutupora ya Singida. Matarajio yetu ni kwamba kabla Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kabla hajamaliza awamu yake ya pili, azindue reli inayotoka Dar es Salaam hadi Mwanza,” alisema.
Kuhusu kipande cha kutoka Uvinza hadi Musongati (Burundi) na Uvira (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo), Waziri Mkuu alisema: “Upembuzi yakinifu unaendelea kwa kipande cha Uvinza - Kigoma - Musongati - Gitenga - Kindu - Uvira (DRC). Itakapokamilika, reli hii itakuwa ya kwanza kwa urefu barani Afrika na ya tano kwa urefu duniani.”
Alisema miradi ya bomba la mafuta inaendelea, reli ya kutoka Mtwara hadi Mbamba Bay badi inatafutiwa mkandarasi na kusisitiza kwamba katika sekta ya maji vijiji vilivyobakia ni chini ya 1,000. Kuhusu umeme, alisema Serikali imekwishamilisha kuweka umeme katika vijiji vyote na kwamba sasa iko kwenye vitongoji na maeneo ya ujazilizo. Na pia inaendeleza kampeni ya nishati safi ya kupikia.
Kuhusu elimu, Waziri Mkuu alisema inaendelea na maandalizi ya elimu ya lazima itakayoanza kutolewa ifikapo Januari, 2028. “Ikifika mwaka 2028, elimu ya lazima itakua hadi kidato cha nne badala ya ile ya darasa la saba kwa sasa ambapo wanafunzi 3,021,177 watajiunga na kidato cha kwanza.”
“Kwa sasa, tunaendelea na maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa, maabara na karakana. Ili kukidhi mahitaji ya mtaala mpya, tunahitaji maabara 80,000, madarasa 16,000 na walimu wa kutosha,” alisema.
Kwenye sekta ya afya, Waziri Mkuu alisema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kufanya ukarabati wa hosptitali, ujenzi wa vituo vya afya na zahanati nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwezesha kupata huduma bora katika umbali mfupi.
“Serikali ya amwamu ya sita imafanya uwekezaji mkubwa kwa kuongeza upatikanaji wa vifaa tiba ambavyo zamani vilikuwa vinapatikana nje ya nchi au katika hospitali ya Taifa pekee. Kwa sasa, vipimo kama MRI, CTScan na Ultrasound vinapatikana kuanzia Hospitali za Wilaya,” alisema.
Kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini, Waziri Mkuu alisema DIRA 2050 imeweka bayana azma ya ku ifikisha Tanzania kwenye ngazi ya juu ya maendeleo, yaani kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu utakaoongozw a na maarifa na maendeleo ya v iwanda.
Alisema Serikali peke yake haiwezi kutekeleza dira hiyo bali jukumu kubwa linalofanywa na Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa uchumi. “Fursa nyingi zipo katika sekta za madini, kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na uchumi wa bluu. Tunawahitaji Watanzania wote walioko nyumbani na walioko nje kuchangia katika ajenda hii kubwa ya maendeleo,” alisisitiza.
Dkt. Mwigulu ambaye amemaliza ziara ya kikazi ya siku tano nchini Uingereza, alikuwa ameambatana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angella Kairuki, Makatibu Wakuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Uchumi wa Bluu, Watendaji Wakuu wa TISEZA na ZIPA.

Kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini, Waziri Mkuu alisema DIRA 2050 imeweka bayana azma ya ku
Alisema Serikali peke yake haiwezi kutekeleza dira hiyo bali jukumu kubwa linalofanywa na Serikali ni kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa uchumi. “Fursa nyingi zipo katika sekta za madini, kilimo, mifugo, uvuvi, utalii na uchumi wa bluu. Tunawahitaji Watanzania wote walioko nyumbani na walioko nje kuchangia katika ajenda hii kubwa ya maendeleo,” alisisitiza.
Dkt. Mwigulu ambaye amemaliza ziara ya kikazi ya siku tano nchini Uingereza, alikuwa ameambatana na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angella Kairuki, Makatibu Wakuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji pamoja na Uchumi wa Bluu, Watendaji Wakuu wa TISEZA na ZIPA.
No comments:
Post a Comment