Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wakisaini Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreement-DTA), kati ya mataifa hayo mawili, tukio lililofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wakionesha hati za Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreement-DTA), kati ya mataifa hayo mawili, mara baada ya kusaini hati hizo katika tukio lililofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wakibadilishana hati za Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreement-DTA), kati ya mataifa hayo mawili, mara baada ya kusaini hati hizo katika tukio lililofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Na Benny Mwaipaja, DOHA QATAR
TANZANIA na Qatar, leo tarehe
29 Septemba, 2026, zimetia saini Mkataba wa Kuepusha utozaji kodi mara mbili na
kuzuia ukwepaji kodi (Double Taxation Agreement).
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) na Waziri wa Fedha wa
Qatar, Mhe: Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wamesaini Mkataba huo kando ya Mkutano wa
11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia
(AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Mhe. Balozi Omar amesema kuwa
hatua hiyo imelenga kuboresha mazingira ya biashara kati ya mataifa hayo
mawili, hatua itakayo kuza zaidi uchumi wa pande zote mbili.
"Mkataba huu unaakisi
urafiki imara uliopo kati ya mataifa yetu mawili, pamoja na azma yetu ya
kujenga mfumo wa kisasa, wenye usawa na unaovutia wawekezaji, unaoendana na
viwango vya kimataifa." Alisema Mhe. Balozi Omar.
"Kwa kuondoa utozaji kodi
mara mbili, mkataba huu utachagiza biashara ya kimataifa, uwekezaji na shughuli
za kibiashara. Pia utajenga mazingira ya uwazi na yanayotabirika zaidi kwa
wawekezaji," alisema Mhe. Balozi Omar.
Aliongeza kuwa, mkataba huo
unaimarisha ushirikiano kati ya mamlaka za kodi za nchi zote mbili na utasaidia
juhudi za kimataifa za kupambana na ukwepaji na upunguzaji wa kodi, pamoja na
kulinda maslahi ya kodi ya nchi zote mbili.
Alitaja sekta ambazo Tanzania
inatarajia kuvutia uwekezaji mpya kuwa ni pamoha na miundombinu, nishati,
utalii, usafirishaji na vifaa, kilimo na huduma za fedha.
"Tanzania inautazama
mkataba huu kama fursa ya kuvutia uwekezaji mpya katika sekta mbalimbali"
alisema Mhe. Balozi Omar
Aidha, alizishukuru timu za
kiufundi, wataalam wa kodi, washauri wa kisheria na maafisa wa serikali kutoka
nchi zote mbili, akisema kujitolea kwao ndiyo kumewezesha mafanikio hayo.
Aliongeza kuwa nchi zote mbili
sasa zinatazama utekelezaji wa haraka wa mkataba huo na ushirikiano wa kiuchumi
uliozidi kuwa wa kina kwa manufaa ya pamoja ya wananchi wa nchi zote mbili.
Kwa upande wa biashara,
alisema kuondolewa kwa utozaji kodi mara mbili katika mapato, kunatarajiwa
kupunguza gharama za uendeshaji kwa kampuni zinazofanya kazi katika nchi zote
mbili, na kuweka mazingira ya uhakika zaidi kwa wawekezaji wanaotaka kupanua
shughuli zao katika mataifa hayo.
Kwa upande wake, Waziri wa
Fedha wa Qatar, Mhe: Ali Bin Ahmed Al Kuwari, alisema kuwa Tanzania ni mshirika
muhimu wa kiuchumi wa Qatar na kwamba kuondolewa kwa vikwazo vya utozaji kodi
mara mbili katika mapato yanayotokana na biashara zinazofanyika kati ya mataifa
hayo mawili kutavutia zaidi uwekezaji na mitaji kutoka katika nchi hizo.
Amesisitiza nia ya nchi yake
kuendeleza ushirikiano wa karibu na Tanzania, akibainisha kuwa Mamlaka ya
Uwekezaji ya Qatar (QIA) na Mfuko wa Maendeleo wa Qatar (QFFD) tayari
wanashiriki katika miradi mbalimbali nchini humo.
Alieleza utayari wa Qatar
kusaidia katika ubadilishanaji wa maarifa na utaalamu, badala ya kuhamisha
maarifa pekee.
Mhe: Ali Bin Ahmed Al Kuwari
aligusia umuhimu wa ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi na kwamba kuwepo
kwa mikataba ya kuzuia utozaji kodi mara mbili ni muhimu kwa miradi
iliyotekelezwa tayari nchini Tanzania na miradi mipya kutoka nchi hizo mbili.
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wakionesha hati za Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreement-DTA), kati ya mataifa hayo mawili, mara baada ya kusaini hati hizo katika tukio lililofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Qatar, Mhe. Ali Bin Ahmed Al Kuwari, wakibadilishana hati za Mkataba wa kuondoa utozaji kodi mara mbili (Double Taxation Agreement-DTA), kati ya mataifa hayo mawili, mara baada ya kusaini hati hizo katika tukio lililofanyika kando ya Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Miundombinu ya Asia (AIIB) uliofanyika jijini Doha nchini Qatar.
Na Benny Mwaipaja, DOHA QATAR
.jpg)

.jpg)

.jpg)

No comments:
Post a Comment