Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemtaka Msajili wa Hazina kuandaa
tuzo itakayotambua Taasisi au Shirika lililofanya vizuri zaidi katika kuajiri
na kuwezesha mafunzo kwa vijan.
Makamu wa Rais ametoa wito
huo, wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na
Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, kilichofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Tarehe 28 Septemba 2026.
Aidha, Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ili
kufanikisha nguzo tatu za Dira ya Taifa 2050 ni muhimu Taasisi na Mashirika ya
Umma kuaandaa vijana ili waweze kushindana katika soko la ajira.
Makamu wa Rais amesema hayo,
wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji
Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Tarehe 28 Septemba 2026.


No comments:
Post a Comment