Ameyasema hayo tarehe 8 Machi 2026, katika Mji wa Laela, Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba iliyoanza jana mkoani Rukwa.
“Kwa
maelekezo ya Rais, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na maelekezo yako, tunaendelea kuhakikisha
inapofika mei 2026 tunawasha umeme kupitia mradi wa TAZA. Hali ya mradi inaenda
vizuri na kama kila kitu kitakwenda kama kilivyo, itakapofika mwezi wa tano
mwaka huu hatimaye Mkoa huu wa Rukwa utanufaika na umeme wa gridi.” Amesema
Mhe.Salome
Ameeleza
kuwa, kwa sasa mkoa wa Rukwa unapata umeme kutoka nchini Zambia kupitia
mashirikiano ya biashara ya umeme katika nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (Southern
Africa Power Pool) ambayo yanawezesha nchi wanachama kuuza au kununua umeme pale
kunapokuwa na uhitaji ili kukidhi mahitaji ya wananchi.
Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, amesema jitihada mbalimbali zinaendelea ili kuweza kufikia asilimia 80 ya wananchi wanaotumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo 2034 ikiwemo ya kusambaza majiko banifu na mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku.

No comments:
Post a Comment