Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliyofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 07 Novemba 2025, Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akishiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, uliyofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 07 Novemba 2025, Dodoma.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kurejesha
utengamano katika nchi na kuhakikisha wananchi wanaishi katika utawala wa
sheria.
Makamu wa Rais amesema hayo
wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), uliyofanyika kwa
njia ya mtandao, akiwa mkoani Dodoma.
Amesema dhamira ya Rais Dkt.
Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha mchakato wa mazungumzo ya maridhiano
unafanikiwa ili kuwa na Taifa lenye amani na umoja na kuendelea kuwa mfano wa
utulivu katika Afrika na Dunia kwa ujumla.
Halikadhalika, Makamu wa Rais
amesema Tanzania ni salama na tulivu na ipo tayari kuendelea kupokea wageni
kutoka duniani kote kwa manufaa ya nchi zote.
Aidha, Makamu wa Rais,
amewashukuru viongozi wa SADC walioshiriki uapisho wa Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan pamoja na wote waliotoa pongezi za dhati. Amesema jitihada zote zitatumika
kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amani kuendelezwa.
Mkutano huo umempongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushindi
aliyoupata na uchaguzi wenye mafanikio.
Mkutano huo ulilenga kujadili kujiondoa
kwa nchi ya Madagascar kama nchi Mwenyekiti wa SADC, ambapo nchi ya Afrika
Kusini imependekezwa kuwa Mwenyekiti kwa kipindi cha mpito mpaka kufikia mwezi
Agosti 2026.
Mkutano huo umekubaliana
kuendelea kutumia kauli mbiu ya Mkutano wa 45 wa SADC uliyofanyika nchini
Madagascar ambayo ni “Kuimarisha Viwanda, Mapinduzi ya Kilimo, Mabadiliko ya
Nishati kwa SADC yenye Uhimilivu”
0 comments:
Post a Comment