June 29, 2025

JAJI MKUU MSTAAFU PROF IBRAHIM JUMA ATEULIWA MKUU MPYA WA CHUO UDOM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:- 

i. Jaji Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Mheshimiwa Prof. Juma anachukua nafasi ya Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; na 
ii. Dkt. Deo Mwapinga ameteuliwa kuwa Balozi. Dkt. Mwapinga ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wabunge wa Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR).

No comments:

Post a Comment