Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2025







WACHIMBAJI wadogo wa Mgodi wa Dhahabu wa Basia uliopo kijiji cha Mwanubi Wilaya ya Shinyanga Vijijini wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea huduma ya umeme katika mgodi huo.

Akizungumza Mwenyekiti wa Mabroka Mkoa wa Shinyanga (CHAMATA) Masanja Meja  amesema kupitia Tume ya Madini imewasaidia  kupata miundombinu ya umeme katika mgodi huo na wameweza kuokoa  gharama za uendeshaji kwa zaidi ya asilimia 70.

“Umeme unatusaidia sana katika uchenjuaji, siku za nyuma kwa siku  tulikuwa tunatumia lita 20 za dizeli ambayo kwa siku si chini ya shilingi  70,000  kwa mwezi ni Shilingi  milioni 2.1 lakini kwa sasa tunatumia umeme wa Shilingi 15,000 kwa siku kwa mwezi ni Shilingi 450,000 kwetu ni nafuu kubwa,”amesema Meja.

Aidha, amesema kutokana na miundombinu hiyo ya umeme uzalishaji umeongezeka kutoka  gramu 300 kwa mwezi  mpaka gramu 800 hivyo kuongeza pia mapato ya serikali.

Naye Katibu wa Mgodi wa Basia, Gaga Lupande amesema mgodi huo umekuwa ukishirikiana na wananchi katika shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo uboreshaji wa shule ya msingi  Mwanubi pamoja na ujenzi wa Zahanati unaoendelea.

Amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo  itaweza kuhudumia Kaya 500  zilizopo katika eneo hilo na kuondoa adha ya  wananchi hao kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Posted by MROKI On Thursday, March 13, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo