Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki swala ya kumuombea Marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile, aliposhiriki maziko yaliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya, Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi Februari 22, 2025.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile, aliposhiriki maziko yaliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya, Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi Februari 22, 2025.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumzaa na waombolezaji aliposhiriki maziko Marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile yaliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya, Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi Februari 22, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa pole Mzee Abdalah Saidi Nchamala kutokana na kifo cha mkewe Marehemu Asina Omary Nyimbilile, aliposhiriki maziko yaliyofanyika kwenye makaburi ya Jumuiya, Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi Februari 22, 2025.
****************
WAZIRI MKUU na Mbunge wa Jimbo ya Ruangwa Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Februari 22, 2025 ameshiriki katika mazishi ya marehemu Bi. Asina Omary Nyimbilile mkazi wa Kata ya Nkowe, Ruangwa mkoani Lindi.
Akizungumza na waombolezaji katika mazishi hayo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka ndugu, jamaa na marafiki kumuombea Marehemu Bi. Asina pumziko la milele pamoja na kuyaenzi yote mema aliyofanya wakati wa uhai wake.
Bi. Asina amezikwa katika makaburi ya jumuiya yaliyopo katika kata ya Nkowe.
Mazishi hayo pia yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Ndugu Hassan Jarufu, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hassan Ngoma na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ruangwa Ndugu Ibrahim Ndoro.
0 comments:
Post a Comment