February 24, 2025

WAZIRI KIKWETE KUFANYA ZIARA YA SIKU TATU MKOANI SONGWE





Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu -Mhe. Ridhiwani Kikwete leo Februari 23, 2025 amewasili mkoani Songwe kwa lengo la ziara ya  kukagua miradi ya Maendeleo ikiwemo ya sekta  ya Elimu, Afya na Miundombinu   kwa ajili ya ustawi wa maendeleo ya wananchi .

Mhe. Waziri Kikwete anatarajiwa kukagua na kuweka Mawe ya msingi katika miradi hiyo ambayo inakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 700 katika Halmashauri zote za mkoa huo.

Mara baada ya kuwasili katika  mkoa huo , Waziri Kikwete alipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Daniel Chongolo ambaye alimpa hali ya maendeleo ya Mkoa huo na maandalizi ambayo yameshafikiwa kwa ajili ya ziara hiyo.

Vile vile Mhe.  Kikwete anatarajiwa pia kukagua Maendeleo ya Kituo cha Vijana cha Sasanda wilayani   Songwe ambapo atakagua  mradi wa Shamba la vijana lililopo kituo hicho.

 Mhe Waziri Kikwete ameambatana  na watendaji mbalimbali ambapo amemhakikishia Mkuu wa mkoa huo  kuwa timu yake iko tayari kwa ajili ya kazi iliyowaleta.

No comments:

Post a Comment