Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiifariji familia ya aliyeshiriki tukio la
kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael
Mushi. Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akiifariji familia ya aliyeshiriki tukio la
kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael
Mushi. Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja akisaini kitabu cha maombolezo alipowasili eneo
la Makongo Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025 kwa ajili ya kutoa pole
na kuifariji familia ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa
Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia
Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati) akiwa katika katika picha ya pamoja
na familia ya Marehemu Sifael Mushi aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa
iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo
Februari 22, 2025.
Sehemu ya waombolezaji
nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha aliyeshiriki tukio
la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar Marehemu Bi. Sifael
Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Cypriana Luhemeja (katikati) akiwa katika akiwa na Naibu Karibu
Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi (wa pili kulia), Mkurugenzi wa
Muungano Dkt. Juma Mohamed Salum na ndugu wa Marehemu Sifael Mushi aliyeshiriki
tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, wakati wa
ibada ya fupi nyumbani Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo Februari 22, 2025.
Ametoa wito huo wakati
akizungumza na waombolezaji eneo la Makongo Juu Jijini Dar es Salaam leo
Februari 22, 2025 Jijini Dar es Salaam, alipofika kutoa pole na kuifariji familia
ya aliyeshiriki tukio la kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar
Marehemu Bi. Sifael Mushi ambaye amefariki dunia Februari 20, 2025.
Akitoa salamu za Serikali,
Mhandisi Luhemeja amesema Marehemu Sifael alikuwa ni mtu muhimu katika historia
ya Muungano wakati wa tukio la kuchanganya udongo lililkofanyika Aprili 26,
1965 ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuasisiwa kwa Muungano Aprili 26, 1964.
Akiifariji familia ya marehemu
amesema pamoja na majonzi ya kumpoteza mpendwa wao, ina bahati ya kupata mtu
aliyeshuhudia Muungano ambao umedumu hadi leo.
“Niwaombe tuudumishe Muungano
kwani wengi wetu tumezaliwa baada ya Muungano hivyo ni vyema tukaendelea
kuitunza historia yake namna alivyoshiriki katika tukio lile la kuchanganya
udongo, ni nadra sana kumuona Mtanzania mmoja ana picha ya Rais wa Awamu ya Sita,
wa Awamu ya Tano, Awamu ya Nne na Awamu ya Kwanza si jambo rahisi, lakini kwa
Marehemu Sifael tunalishuhudia,” amesema.
Marehemu Sifael ambaye alikuwa
miongoni mwa vijana wa Kitanzania walishiriki katika tukio la kuchanganga
udongo wa Tanganyika na Zanzibar, alifariki dunia katika Hospitali ya Mzena
Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Wengine walioshiriki katika
tukio hilo na wametangulia mbele ya haki ni Marehemu Hassanieli Mrema
aliyefariki Mei 04, 2024, Marehemu Khadija Abbas Rashid alifariki Agosti 22,
2023 na Marehemu Omar Hassan Mkele alifariki Agosti 28, 2024.
0 comments:
Post a Comment