Nafasi Ya Matangazo

February 05, 2025


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Serera ameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kazi nzuri ya usimamizi wa Vipimo katika Sekta mbalimbali.

Dkt. Serera ameyasema hayo alipotembelea taasisi ya Wakala wa Vipimo katika kituo chake cha uhakiki wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.

Dkt. Serera amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika kituo hicho ambazo ni uhakiki wa mita za umeme, uhakiki wa Dira za Maji pamoja na uhakiki wa matenki ya malori yanayosafirisha vimiminika.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bw. Alban Kihulla amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa ziara yake ambapo ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi na kuendelea kuingia katika maeneo mapya ya usimamizi wa Vipimo kama upimaji wa taxi meter.




Posted by MROKI On Wednesday, February 05, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo