Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akiwatunuku wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) shahada mbalimbali, katika Mahafali ya 10 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akitoa rai kwa wadau wa sekta ya Takwimu Rasmi kushirikiana na Serikali katika kukokotoa viashiria vya maendeleo ili kutathmini hatua zilizopigwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoisha mwaka 2025 wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi, akimwongoza Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipowasili katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Takwimu, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), wakiwa tayari kutunukiwa Shahada mbalimbali, wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Takwimu, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa tatu kushoto), Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Dkt. Tumaini Katunzi (wa tatu kulia) na Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Takwimu, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
******************
Na. Scola Malinga, WF, Dar es SalaamNaibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ametoa rai kwa wadau wote wa sekta ya Takwimu Rasmi kushirikiana na Serikali katika kukokotoa viashiria vya maendeleo ili kutathmini hatua zilizopigwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa inayoisha mwaka 2025 na hatua zilizopigwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu yanayoisha mwaka 2030.
Mhe. Chande, alitoa rai hiyo wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa lengo la wadau wa takwimu rasmi liwe kuhakikisha takwimu zinakuwa rahisi kutumika katika kupanga mipango ya kukuza uchumi, kuboresha huduma za jamii, kutunza mazingira na kupunguza umasikini bila kuwaacha wengine nje.
“Ukuaji wa uchumi wa mmoja mmoja na ubora wa hali ya maisha na mazingira unatarijia mipango bora inayopimika kwa takwimu rasmi, hivyo katika mahafali haya, nakipongeza Chuo kwa kuzalisha wataalam mbali mbali katika tasnia pana ya Takwimu Rasmi na nawasihi kutimiza majukumu yenu kwa weledi ndani ya Taifa, Barani Afrika na duniani kote”, alisema Mhe. Chande.
Akizungumzia suala la matumizi ya kidigitali katika masuala ya takwimu, Mhe. Chande alisema kuwa Serikali tayari imeandaa mazingira kwa wananchi wake na wafanyabiashara kumudu mabadiliko ya kidijitali kwa kuweka anwani za makazi za kidijitali pamoja na maboresho ya teknolojia ya mawasiliano yanayorahisisha upatikani wa taarifa za sensa na tafiti ndogo katika ngazi ya vitongoji, mitaa na shehia.
Mhe. Chande alisema kwa wadau wa sekta binafsi hususani rika la vijana, walio masomoni, wahitimu na walioko makazini, wanatakiwa kuwekeza zaidi katika sekta ya ubunifu wa mifumo ya biashara dijitali na kilimo cha kisasa.
Aidha alitoa shukrani kwa Kamisheni ya Uchumi Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA), waheshimiwa mabalozi, maofisa wakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, washirika wa maendeleo, wakurugenzi wakuu wa Ofisi za Taifa za Takwimu za nchi wanachama wa Chuo na wadau wengine wanaoshirikiana na Chuo kwa kuwa kunawezesha kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kitaifa, kikanda na kimataifa.
No comments:
Post a Comment