November 10, 2024

WAJUMBE WA KAMATI YA ARDHI WAIPONGEZA WIZARA YA ARDHI KWA MRADI WA MJI WA AFCON ARUSHA

Na Mwandishi Wetu, Arusha 
Kamati ya Bunge ya  Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga  Sh. bilioni 8 kwa ajili ya kuanza kutelekeza  Mradi wa Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) katika eneo lililopo pembezoni mwa uwanja wa mpira wa Afcon unaojengwa Kata ya Olmort  Jijini Arusha.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki Novemba 10, 2024 Jijini Arusha na  Makamu   Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Najma  Murtaza Giga wakati kamati hiyo ilipotembela na kujionea eneo la mradi wa KKK pamoja na kujionea ujenzi wa uwanja  wa Afcon unaojengwa kwa ajili ya mashindano  ya Mpi mwaka 2027.

Aliipongeza serikali kupitia Wizara ya Ardhi  kwa kuja na mradi huo wa viwanja na kuongeza kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwani ndani ya miaka miwili ya ujenzi wa uwanja huo wa Afcon si mbali hivyo serikali iharakishe ujenzi huo huko makazi ya wananchi yakipimiwa na kuanishwa shughuli mbalimbalimbali za maendeleo 

"Hii ni historia na Arusha inahistoria yake kwa utalii na fursa zingine hivyo tunahitaji taarifa kamili juu ya mradi huu ili tuweze kuishauri serikali katika kuhakikisha vipaumbele vya awali vinapatikana na fursa za uwekezaji zinakuwepo kwani Afcon haipo mbali lazima tujipange kwani eneo hili la viwaja si mbali na mji na Jiji la Arusha litapendeza sana mara mradi huu utapokamilika"

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba  na Maendeleo ya Makazi, Deo Ndejembi alisema fedha hizo zimetolewa na wizara hiyo kwaajili ya ulipaji wa ekari 207 za awali kati ya ekari zaidi ya 4,575.5 zilizopo katika mpango wote huo ambapo uwanja wa Afcon pekee unakeri 83 .

"Wizara imetenga fedha hizi kwaajili ya kuanza ulipaji fidia na tunategemea tukimaliza kupima viwanja hivi tutanunua vingine hapo badae kadri wizara itakavyooata hela kwaaajili ya kupima ,kupanga na Kumilikisha lengo letu mji wa Arusha na maeneo mengine nchi nzima yapangwe badala ya kuwa na maeneo yasiyopangwa"

Wakati huo huo, Naibu  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Pinda alisema Arusha ni mji wenye historia ya aina yake hivyo lazima mipango sahihi iwepo katika kuondoa mji katika maeneo yasipoangwa hadi iwe iliyopangwa na kuwasihi wananchi wa mkoa huo wawe na subra wakati serikali ikipanga mji huo na kuipongeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwakuhakikisha mji unapangwa na kuwa na Maendeleo zaidi

"Tupo makini kuhakikisha mji unajengwa na  uwanja wa Afcon ukiisha hapa tutakuwa na makazi yenye mpangilo bora na wa aina yake"

Huku Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye ni  mbunge kutoka Tabora, Emmanuel Mwakasaka  alipongeza wizara hiyo kwa kuja na mkakati huo wa upimaji maeneo  maeneo nchi nzima na kumshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa Uwanja huo wa Afcon ambao utawezesha Mkoa wa Arusha kupaa zaidi kimapato.

Awali akiwakaribisha wajumbe wa kamati hiyo na watendaji wa Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema wizara imepanga kuhakikisha mji wa AFCON umepangwa vizuri ili kupendezesha mji wa Arusha kuendelea kuwavutia kulipendezesha jiji hilo kwa kupangwa na kuondoa makazi holela.









No comments:

Post a Comment