Wachezaji Musa Chilendi wa Wizara ya Uchukuzi na Niuka Chande wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wametwaa ubingwa wa mchezo wa draft kwa wanawake na wanaume katika michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) inayofanyika mkoani Morogoro.
Musa mchezaji chipukizi amemfunga mkongwe Gervas Mwashimaa wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika mchezo mkali wa fainali kwa pointi 2-1.
Ushindi wa tatu kwa wanaume umechukuliwa na Ishengoma Kiliba wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliyemfunga Ishara Charles wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa pointi 1-0.
Kwa upande wa wanawake Niuka wa Mawasiliano amemfunga mpinzani wake Pulkeria Maimu wa TAMISEMI kwa pointi 2-1. Wachezaji hawa walikutana fainali katika michezo ya mwaka 2023 na Niuka akaibuka bingwa.
Ushindi wa tatu kwa wanawake umechukuliwa na Badaka Kabaka wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyemfunga Mizowa Wemena wa Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment