Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuwasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya kwa lengo la kuzindua shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipiga makofi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Rorya wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Aliyevaa kofia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi.
Mwonekano wa madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri iliyozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Wa pili kutoka kushoto) akisisitiza jambo wakati akielekea kuweka jiwe la msingi katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Rorya alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mara. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evance Mtambi na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Dkt. Khalfan Haule.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri mara baada ya kuzindua shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kuzindua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Rorya.
**************
Na. Veronica Mwafisi-RoryaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amezindua Shule ya Sekondari ya Kutwa Ingri huku akiwasisitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii kwa maendeleo yao ya baadae na taifa kwa ujumla.
“Shule nzuri namna hii kujengwa kijijini ni maendeleo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, hivyo ni wajibu wenu ninyi wanafunzi kusoma kwa bidii kwa maendeleo yenu na taifa kwa ujumla,’’Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Ingri umeigharimu Serikali kiasi cha shilingi milioni 584 mpaka kukamilika kwake ambapo inajumuisha madarasa, maabara, chumba cha TEHAMA na Maktaba.
Ujenzi wa shule hiyo umewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi hao na kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule waliokuwa wakisoma awali.
Mhe. Simbachawene amewasisitiza wanafunzi na watumishi wa shule hiyo kutunza majengo na vifaa vyote vilivyomo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amezindua ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya utakaotumika kufanya shughuli mbalimbali kwa maendeleo ya Halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment