September 26, 2024

U T E U Z I : RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

i. Bw. David Chimbi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL);

ii. Balozi Dkt. Aziz Ponary Mlima ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO);

iii. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Salim Milanzi ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania;

iv. Balozi Valentino Longino Mlowola ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF);

v. Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo (TEMDO); na


vi. Prof. Neema Mori ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment