September 01, 2024

RAIS NA AMIR JESHI MKUU SAMIA ASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA JWTZ

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Taasisi za kidini zina wajibu mkubwa katika kulinda misingi ya familia na kujenga Taifa lenye maadili.
 
Rais Dkt. Samia amesema hayo leo katika hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya kusoma Quran Tukufu kwa wasichana, yaliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana Taasisi ya World Muslim League ya Saudi Arabia, yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
 
Aidha, Rais Dkt. Samia ametoa wito kwa BAKWATA kuweka mikakati ya kufundisha elimu ya dini kwa watoto wote bila ubaguzi na kusisitiza umuhimu wa elimu ya dini kwa wanawake kwa kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika ulezi wa familia bora.
 
Vile vile, Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa, kumlea mtoto wa kike katika misingi mizuri ya kiimani kunamuandaa kuishi katika misingi hiyo. Hivyo, ni muhimu kuendelea kuimarisha familia ambayo ni msingi wa Taifa letu, ikiwemo kupitia elimu ya dini.
 
Akizungumzia mashindano hayo yaliyofanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa, kuchanguliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa kwanza wa mashindano hayo ni kutokana sifa kubwa ya Tanzania ya kuishi kwa amani na masikilizano.
 
Rais Dkt. Samia amewataka Watanzania waendelee kulinda heshima hiyo kwa kudumisha amani na mshikamano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipiga saluti wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride rasmi la miaka 60 la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024.
Mtukio mbalimbali  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 kwa Jeshi hilo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024.


Mtukio mbalimbali  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 kwa Jeshi hilo katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Kitabu cha miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Septemba, 2024.














No comments:

Post a Comment