July 12, 2024

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA UJENZI WA MNARA WA MASHUJAA DODOMA





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2024 amekagua  ujenzi wa Mnara wa Mashujaa  uliopo mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni  maandalizi ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika Dodoma, Julai 25, 2024.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mnara huo Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi na amemtaka mkandarasi wa mnara huo ambaye ni Suma JKT kukamilisha ujenzi kwa viwango na ubora ifikapo Julai 22 mwaka huu.

Naye, mshauri elekezi kiongozi, Dkt. Ladislaus Mrema amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa eneo hilo la mnara unajumuisha ujenzi wa uwanja wa gwaride, ngazi, njia za watu wenye mahitaji maalum pamoja na kitako cha mnara na bushati eneo la kuzunguka mnara “Mpaka  sasa mradi huu umefikia asilimia 84”

Siku ya Mashujaa itafanyika Julai 25, mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment