Nafasi Ya Matangazo

July 04, 2024





Tume ya Madini leo Julai 03, 2024 imeendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea  jijini Dar es Salaam.

Elimu imetolewa katika maeneo ya usimamizi/udhibiti wa Sekta ya Madini na ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na tozo mbalimbali zinazotokana na shughuli za madini, utoaji na usimamizi wa leseni za utafutaji wa madini, uchimbaji na biashara ya madini pamoja na namna ya kujisajili katika mfumo wa Online Mining Cadastre Transaction Portal (OMCTP),ukaguzi na usalama wa migodi, afya, mazingira na njia bora ya uzalishaji wa madini kwa migodi midogo, ya kati na mikubwa.

Maeneo mengine ni pamoja na usimamizi wa biashara ya madini inayofanyika katika masoko ya madini yaliyoanzishwa nchini, ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini na wajibu wa wawekezaji kwa jamii  katika uboreshaji wa huduma (Corporate Social Responsibity; CSR)

Aidha,  elimu imelenga katika maeneo ya upatikanaji wa vibali mbalimbali vya kusafirisha madini ndani na nje ya nchi  na huduma zinazotolewa na  Maabara ya Tume ya Madini hususan upimaji wa madini ya metali.

Wakizungumza wadau mbalimbali waliotembelea banda la Tume ya Madini wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini kupitia utoaji na usimamizi wa leseni za madini, usimamizi wa masoko ya  madini na vituo vya  ununuzi wa madini nchini, usimamizi wa usalama kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta  ya Madini.

Wakati huohuo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse ametembelea banda la Tume ya Madini na kuwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu na uzalendo ili Sekta ya Madini iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi.
Posted by MROKI On Thursday, July 04, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo