July 31, 2024

TANZIA: MWANDISHI WA HABARI THEOPISTA NSANZUGWAKO WA TSN AFARIKI DUNIA

Marehemu Theopista F. Nsanzugwako

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN),wachapishaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HabariLEO, HabariLEO Jumapili na SpotiLEO, Bi. Asha Dachi anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi, Bi. Theopista Firdbert Nsanzugwako, Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Gazeti la HabariLEO mkoani Dar es Salaam, kilichotokea tarehe 31.07.2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa anapatiwa matibabu.

Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na Ofisi ya  Mkurugenzi Mtendaji kwa kushirikiana na familia ya marehemu. 

TSN inatoa pole kwa watumishi wake wote, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na msiba huu mzito.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, apumzike kwa amani. AMINA.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano Kwa Umma na Nyaraka.

No comments:

Post a Comment