Mratibu wa mradi wa HEET upande wa elimu
jumuishi, Dkt. Perpetua Kalimasi (kushoto), akimkabidhi Bi. Agnes Lugwisha
(kulia) miwani Maalumu ya kusomea (optical carson) iliyotolewa kupitia mradi wa
HEET.
***********
Chuo Kikuu Mzumbe ni moja ya taasisi za elimu ya juu zinazotekeleza Mradi wa HEET ambao umeendelea kufanya mageuzi ya kimaendeleo chuoni hapo.Kupitia mradi huo leo tarehe 23.01.2024, Mratibu wa Mradi wa HEET upande wa Elimu Wezeshi Dkt. Perpetua Kalimasi amekabidhi vifaa muhimu kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu vitakavyowawezesha katika masomo yao.
Vifaa vilivyokabidhiwa kwa wanafunzi ni pamoja na Bajaji, simu za mkononi, kompyuta mpakato na miwani ya kuongeza uoni (optical carson).
Dkt. Kalimasi amewasisitiza wanafunzi hao kuvitunza vifaa hivyo maana vinanunuliwa kwa gharama kubwa.
Pia, Naibu Mshauri wa Wanafunzi Bw. Alphoncy Kauki amewaeleza wanafunzi hao kuwa wajione sawa na wenzao katika muda wote watakapokuwa katika masomo yao na kusisitiza kuwa Chuo kinawajali na kinategemea kuwa watafaulu vizuri na kulitumikia taifa huko mbeleni.
Naye Waziri wa Jinsia na Watu wenye Uhitaji maalumu wa Serikali ya Wanafunzi Bi. Gloria Martin Mwakalembusya ameishukuru serikali kupitia mradi wa HEET kwa kuwawezesha wananafunzi hao na kutoa rai ya kutunza vifaa hivyo ili viwe chachu ya kufanikiwa kati masomo yao.
No comments:
Post a Comment