Waziri
wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na
wananchi wa Lihuli mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kitai-Lihuli (km
84.5), sehemu ya kwanza Amani Makoro - Ruanda (km 35) kwa kiwango cha lami na
sehemu ya pili Ruanda – Ndumbi Port (km 50), inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango
cha lami, Mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Lihuli mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kitai-Lihuli (km 84.5), sehemu ya kwanza Amani Makoro - Ruanda (km 35) kwa kiwango cha lami na sehemu ya pili Ruanda – Ndumbi Port (km 50), inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani Ruvuma.Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akimshukuru Mbunge wa jimbo la Nyasa, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Lihuli mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kitai-Lihuli (km 84.5), kwa kiwango cha lami, Mkoani Ruvuma.
Mbunge wa jimbo la Nyasa, Mheshimiwa Mhandisi Stella Manyanya, akizungumza na wananchi wa Lihuli mara baada ya kukagua ya ujenzi wa barabara ya Kitai-Lihuli, (km 84.5), kwa kiwango cha lami, Mkoani Ruvuma.
Wananchi
wa kijiji cha Lihuli wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (hayupo
pichani) kwenye mkutano wa hadhara mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya
Kitai-Lihuli (km 84.5), kwa kiwango cha lami, Mkoani Ruvuma.
************
Serikali
imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 96 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya
Lituhi kuelekea Bandari ya Ndumbi yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha
lami.Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa leo tarehe 25 Januari 2025 wakati akizingumza na wananchi wa Lituhi mara baada ya kukagua barabara hiyo ambayo ipo katika hatua za kusainiwa mkataba.
Bashungwa amesema ujenzi wa barabara hiyo utawezesha meli za mizigo hasa makaa ya mawe ziweze kupakia kupitia Bandari ya Ndumbi kwenda sehemu mbalimbali za nchi yetu na nchi jirani za Malawi na Msumbiji.
Ameongeza kuwa barabara hiyo inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Daraja la Ruhuhu ambayo itafungua fursa za maendeleo na biashara.
Bashungwa ameagiza Wakala wa Barabara (TANROADS), kumsimamia Mkandarasi atakayepatikana kwa karibu ili mradi huo ukamilike kwa viwango.
Kwa upande wake, Mbunge wa Nyasa, Mhe. Eng. Stella Manyanya, amemuomba Waziri huyo kuwajengea angalau madaraja maeneo korofi hasa katika vipindi vya mvua kwani imekuwa Kero kwa wananchi wake.
Eng. Manyanya ameomba kipande cha barabara kutoka Mbambabay hadi Chiwimbi (km 45) ipewe kipaumbele kwa kuwa ni barabara muhimu na ya Ulinzi ambayo inaunganisha nchi ya Tanzania na Msumbiji, hivyo anaomba ipewe kipaumbele.
“Barabara ya kutoka Nyoni- Matomoni haimo kwenye ilani ila tulikuwa tunaomba ifanyiwe upembuzi yakinifu kwa sababu ni barabara ya uchumi, Kahama yote inatoka huko” ameongeza Eng. Manyanya.
No comments:
Post a Comment